KAULI YA TUNDULISU

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu

Chadema: Hatujakurupuka kumpendekeza Lowassa

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema chama hicho hakikurupuka kumpendekeza Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuchukua fomu ili kuwania urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Akizungumza leo wakati Lowasaa akichukua fomu hiyo Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam amesema, “ Moja ya kazi ya Kamati Kuu ya chama itakuwa (a) kufanya utafiti wa wagombea urais na wagombea wenza na kuwasilisha ripoti zake kwa Baraza Kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa mkutano mkuu.”
“Tukio la leo ni la kihistoria. Ni ukamilishaji wa utaratibu wa ukamilishaji wa utafiti uliofanyika na chama chetu kwa zaidi ya miezi mitatu. Tumefanya utafiti tunaendaje katika uchaguzi mkuu. Tunajipangaje. Tunahitaji wagombea wa aina gani na wenye nguvu kiasi gani kwa sababu tunataka 25 oktoba mwaka huu ndio uwe mwisho wa utawala wa CCM na mfumo tawala,” amesema Lissu.
Lissu amesema wamefanya utafiti wa kina hata kupata jina la Lowassa. Kazi kubwa imefanyika ila hawakutangaza kwa sababu maalum.
“Katika utafiti wa Kamati Kuu, ulihusisha viongozi wote wakuu wa chama hiki pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya chama na wajumbe wa sekretariet.
“Naposema viongozi wakuu nina maana utaratibu uliotumika kumpata Lowassa ulishirikisha katika hatu zote; mwenyekiti wa chama taifa, katibu mkuu, mkamo wenyeviti wote wawili wa chama, manaibu katibu wakuu wote wawili na wajumbe wote wa kamati kuu ya chama,” ameongeza Lissu.
Aidha, amesema baada ya kazi hiyo Kamati Kuu ilikaa siku ya Jumapili iliyopita katika kikao kilichomalizika saa 6 za usiku. kikao hicho kilifanya uamuzi kwamba, “Mtu anayefaa kupeperusha bendela ya Chadema na kwa maana hiyo bendela ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika uchaguzi mkuu ni Lowassa. Uamuzi huo ulifanywa kwa kina na ukafikiwa baada ya mjadala mrefu na mpana.”
Ameongeza kuwa kwa mila na desturi za Chadema, uamuzi unapofanywa na vyombo halali vya chama kwa kufuata njia zilizowekwa na katiba na taratibu za chama, Kila kiongozi na kila mwanachama anapaswa kuuheshimu na kuutekeleza.

Comments

UNITEC COMPUTER ACCESS