Safari ya vijana wa 3 kutoka nzega
Safari ya vijana wa 3 kutoka nzega waliotembea siku 37 kufikisha ujumbe kwa Rais Kikwete yaishia mikononi mwa Polisi.
Vijana hao ambao walivamia magunia na kusema kuwa wamevaa hivyo
ikiwa ni ishara ya kuonyesha uchungu wa namna ambavyo rasilimali za
taifa zisivyowanufaisha wazawa.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia matembezi hayo wamewataja vijana
hao kama ni wazalendo ambao ujumbe wao unawagusa mamilioni ya
watanzania ambo hawana ujasiri na uwezo wa kufanya kitendo cha kijasiri
kama hicho.
Baada ya vijana hao kufika kwa mkuu wa wilaya walifanya mazungumzo
naye ambapo mkuu huyo aliwtaka wafuate taratibu za kumuona rais na
kusisitiza kuwa matembezi hayo yalipaswa kuishia hapo.
Kufuatia maagizo hayo vijana hao hawakukubaliana na agizo hilo na
kusema wao bado ni yao ya kwenda ikulu Ipo pale pale na ndipo
walipioanza safari nyingine kuelekea huko na kabla ya hapo walitoa
matamko yao mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya kablya ya kukamtwa na
kupelekwa kituo cha polisi magomeni.
Comments
Post a Comment