Lulu Apelekewa Barua ya Uchumba!!

Lulu Apelekewa Barua ya Uchumba!!

Lulu Apelekewa Barua ya Uchumba!!
  • Lulu Apelekewa Barua ya Uchumba!! 1
  • Lulu Apelekewa Barua ya Uchumba!! 2
  • Lulu Apelekewa Barua ya Uchumba!! 3
FUNGUA MWAKA: Mrembo na wigizaji wa Filamu hapa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amepelekewa barua ya uchumba kutoka kwa mfanyabiashara mmoja jijini Dar na kumfanya mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila abaki ameshangaa.Tukio hilo lilitendeka Januari 8, mwaka huu, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako ndiko yaliko makazi ya Lulu na mama yake huyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Risasi,Mshenga amabe inadaiwa  kuwa ni mpambe mkubwa wa mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Isaya, mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam alifika nyumbani  kwa mama Lulu mida ya saa tano asubuhi ambapo alibisha hodi na kufunguliwa na mfanyakazi wa ndani (housegeli) ambapo mshenga alimpa barua hausigeli.
Mara baada ya muda kidogo hausigeli alimrudishia barua mshenga na haya ndio maelezo ya mshenga mara baada ya kukutana na mapaparazi alipouliza kama ni kweli alienda kupeleka barua ya uchumba.
“Kweli nimetoka nyumbani kwao na Lulu, nilipeleka barua ya uchumba ya bosi wangu.
“Nimefurahi nilipofika pale nikagonga geti, akatoka msichana mmoja, nilimuuliza kama mama Lulu yupo akasema yupo, nikampa barua akapeleka maana hakutaka mimi niingie,” alisema mshenga huyo.
“Baada ya muda yule msichana alirudi, akanipa barua akisema eti si ya Elizabeth wala Lulu. Sasa ni ya nani wakati jina la juu ya bahasha ni Elizabeth Michael.”“Naamini kabla mama Lulu hajaisoma aliangalia juu ya bahasha na kuliona jina la Elizabeth Michael ndiyo maana wakati ananirudisha tayari bahasha ilikuwa imefunguliwa.”
Mashenga aliendelea na kusema kuwa taratibu zote ya kuchumbia walizifauta ikiwepo kuweka pasa ya kishika uchumbaTulifuata utaratibu wote, ndani ya bahasha tuliweka shilingi laki moja na zimerudi zote.”
Mama lulu alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu swala hili, mama lulu aliseama,
“Mimi mwenyewe nawashangaa ninyi waandishi. Mambo ya kuolewa anayetakiwa kuulizwa ni Lulu mwenyewe. Kama mtu alileta barua au nini, Lulu ndiyo atajibu.
“Halafu naomba kuwaambia kwamba nilishasema siku nyingi mimi sitaki mambo ya magazeti, hata hao mabosi wenu niliwahi kuwaambia,” alisema mama Lulu na kukata simu.
Lulu mwenyewe alipotafutwa kwa njia ya simu kuhusiana na ishu hii hakupatika.
Jionee picha za mshenga akipeleka baruda ya uchumba hapo juu.
Wajuzi mtuzuje hivi ndivyo watu hufanya wanapotaka kuchumbia?

Comments

UNITEC COMPUTER ACCESS