Kamati mbili zakwama kupata theluthi mbili
25th August 2014
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba,Samia Salum Suluhu.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samia
Salum Suluhu, amesema kamati namba saba na nane zimeshindwa kupata
theluthi mbili, kutokana na uchache wa wajumbe kutoka Zanzibar.
Alisema, tangu mwanzo kamati hizo zimeshindwa kupata theluthi mbili
kutokana na maumbile yao baada ya wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wanachi
kutoka nje.
“Kamati hizo kwa maumbile yao, zina wajumbe wengi kutoka Bara na
wachache kutoka Zanzibar. Kila wanavyopigania kura, hawawezi kufikia
theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar,” alisema Suluhu.
Kwa mujibu wa Suluhu, kwa mazingira hayo watajionyesha kwa jinsi
walivyopiga na kwamba, kwa jinsi Wazanzibari walivyo wachache kwenye
Bunge, ndiyo maana baadhi ya kamati zilipata wajumbe wachache.
Alisema kati ya mambo manne waliyopewa kuyashughulikia baada ya kuleta
mvutano mkali kwenye kamati, wamemaliza suala la Mahakama ya Kadhi na
uraia pacha na kwamba maoni na mapendekezo yao yamepelekwa kwenye kamati
ya uandishi ambayo italinganisha na mapendekezo ya kamati.
Alisema Jumamosi walijadili kwa pamoja suala la Kamati Fedha kati ya Zanzibar na Bara na Muundo wa Bunge.
Alisema wanaendelea kupokea maoni na kwamba licha ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba kusema hatua ya sasa ni kujadili, lakini kanuni za
Bunge hilo zinaruhusu kupokea maoni mapya.
Comments
Post a Comment