LHRC: WATANZANIA WOTE WANA HAKI YA KUJADILI KATIBA,WASIZUIWE!

Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) chenye makao yake jijini Dar Es Salaam,kimewataka wajumbe wa bunge maalum la katiba kuacha tabia ya kuwafumba midomo wananchi wanaotoa maoni yao kuhusiana na mchakato mzima wa kuandika katiba mpya nchini Tanzania.BISIMBA
Akiyasema hayo leo asubuhi akiongea na waandishi wa habari,Mkurugenzi Mtendaji,Dr.Helen Kijo-Bisimba alisema,”Bunge linaposema wananchi waache kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya ni kwenda kinyume na katiba ya nchi yetu,ibara ya 18 na 21 kifungu cha pili”. Alisisitiza kuwa kwenye katiba ya Tanzania, ni haki ya kila raia kutoa ama kupokea taarifa na ni wajibu wake pia kuzitumia taarifa hizo kwa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi-Mtendaji-Ananilea-Nkya
Kwa upande wa Bw.H.Sungusia na Bi.Ananilea Nkya waliongezea kwa kushauri kuwa bunge hili lisimamishwe na lisiendee kwani limekosa uhalali wa kisheria,kisiasa na kuna wasiwasi wa kupoteza pesa nyingi kwenye kitu ambacho kinajulikana wazi kitakataliwa na wananchi.
“Wananchi tusimamie ukweli, tupaze sauti zetu na twende juu ya vyama vyetu,juu ya familia zetu na tuweke maslahi ya nchi mbele”,alisema Bi.Ananilea. Aliyasema hayo akisisitiza kuhusu usimamishwaji wa bunge maalum la katiba na kuwasihi wajumbe hao wajali watanzania kuliko kujali “matumbo yao”. Aliongezea kwa kusema,”anayezorotesha mchakato huu hafai kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi,kwani Rais na Jaji Warioba wameshamaliza kazi zao”
Sungusia   Kwa upande wa kuomba msaada kutoka mahakamani ili kusitisha bunge hilo,mwanasheria Bw.Sungusia alisema ni jambo linalohitaji umakini zaidi kwani ni kama wapo mtegoni. “Ndugu waandishi,kuna kesi nyingi sana zipo mahakamani tangu 2008 lakini hakuna uamuzi uliochukuliwa,tunasita kupeleka suala hili mahakamani kwani hatujui uamuzi wake utatolewa lini na litakuwa na faida na hasara kwa kiasi gani”.
Mkutano huu wa waandishi wa habari uliitishwa na LHRC pamoja wadau wake wa karibu ikiwemo asasi ya vijana ya Tanzania Youth Vision Association (TYVA) iliyowakilishwa na Bw.Naamala Samson ambaye ni mratibu wa mradi wa FURSIKA NA AJIRA.
Unaweza kupakua tamko zima hapa: TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI- MWENENDO MCHAKATO WA KATIBA 7-8-2014
By ijuekatiba

LHRC YATOA MACHAPISHO KUHUSU KATIBA KWA TYVA

LHRC Logo
Katika kutambua mchango wa asasi ya Tanzania Youth Vision Association(TYVA) kuwafikia vijana na kuwaelimisha kuhusu kuifahamu katiba, rasimu za katiba na kuwawezesha kutoa maoni yao kuhusu haki wazitakazo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimetoa machapisho kwenye maboksi zaidi ya 31.
Machapisho kutoka LHRC
TYVA inaendesha mradi wa IJUEKATIBA unaolenga kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wao kwenye kufuatilia mchakato mzima wa katiba. Mradi huu ulioanza tangu mwaka 2011 umeshafikia vijana milioni tano walio kwenye mikoa zaidi ya 18 Bara pamoja na Zanzibar, na inatarajiwa utawafikia walio kwenye mikoa zaidi mijini na vijijini, mashuleni na mitaani kwa njia mbalimbali za midahalo,mafunzo na vyombo vya habari.
Machapisho ya katiba
Randama za Katiba
Shukrani za dhati ziufikie utawala mzima wa Kituo cha Sheria na Haki Za Binadamu kuunga mkono zinazofanywa na TYVA.
By ijuekatiba
Image

JE, UKAWA WATARUDI BUNGENI?

IMG_4681573757244
By ijuekatiba

Comments

UNITEC COMPUTER ACCESS